Mwongozo wa Waelimishaji/Waalimu

Katika ukurasa huu utapata rasilimali ziada kwa ajili ya waalimu na waratibu ikiwa ni pamoja na shughuli, mwongozo wa somo na zana za kufundishia. Rasilimali hizi zimeundwa ili kutoa fursa zaidi za kujifunza kwa vijana ili kuongeza uwezo wao wa kufikiri kwa uangalifu kuhusu teknolojia za dijiti. Tumia rasilimali hizi kando na maonyesho ya What the Future Wants au kama rasilimali huru katika muktadha wowote wa elimu unaoendana na wewe

Shughuli

Habari, rafiki - Shughuli ya kuchora kuhusu muundo unaoshawishi.

Tukabiliane nalo - Jaribio fupi kuhusu teknolojia za kibayometriki

Unafaa? - Shughuli ya kutafakari kuhusu kuongezeka kwa utegemezi wa jamii kwenye teknolojia.

Usiwe mbaya - Kazi ya kutafakari juu ya thamani zinazohusiana na 'big tech'.

Warsha

Kuunda Hadithi ni shughuli ya ubunifu wa pamoja kuhusu vichwa vya habari vya vyombo vya habari na vijana. (Tovuti hii inapatikana kwa Kiingereza pekee.)

Influence the Influencer ni shughuli ya ushirikiano wa kuunda kampeni za haki za kidijitali. (Tovuti hii inapatikana kwa Kiingereza pekee.)

Kile Ambacho Kinakuja ni shughuli ya ushirikiano wa pamoja kuhusu kutabiri mustakabali mbadala wa kidigitali. (Tovuti hii inapatikana kwa Kiingereza pekee.)

Kujadili Dijiti ni shughuli ya mijadala ili kuhimiza mawazo ya kina kuhusu teknolojia. (Tovuti hii inapatikana kwa Kiingereza pekee.)

Nyenzo za ziada

Kuiba Hisia Zako ni programu shirikishi ya kueleza matumizi ya AI ya utambuzi wa hisia katika mitandao ya kijamii.

Data Detox x Youth ni kitabu kazi kinachowezesha wanafunzi kujifunza kuhusu faragha ya data, usalama wa kidijitali, ustawi wa kidijitali na habari potofu. (Tovuti hii inapatikana kwa Kiingereza.)

Ikiwa una nia ya kutumia shughuli hizi, tafadhali wasiliana nasi kupitia youth@tacticaltech.org na tembelea ukurasa wa Andaa "What the Future Wants" yako mwenyewe ili kujua jinsi unavyoweza kushiriki.